Timu ya Azam FC leo December 14 2016 imetangaza kukamilisha usajili wa wachezaji watatu kwa pamoja, Azam FC ambao pia wamethibitisha kuachana na Jean Bapiste Mugiraneza raia wa Rwanda kwa madai kuwa amepata timu Vietnam, imesajili wachezaji watatu wakiwemo wawili wa kimataifa.
Azam FC imewasajili beki wa kati Yakubu Mohammed kutokea Aduana Stars ya Ghana kwa mkataba wa miaka mitatu akiripotiwa kuwa ndio mrithi wa Pascal Wawa, kiungo mkabaji Stephan Kingue Mpondo akitokea Coton Sports ya Cameroon.
Hata hivyo Azam FC pia imekamilisha usajili wa Joseph Mahundi aliyekulia katika Academy yao ya Azam FC na sasa wanamsajili akitokea Mbeya City aliyomaliza nayo mkataba baada ya round ya kwanza kumalizika.
ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0