Usiku wa December 8 2016 Man United walishuka dimbani kucheza mchezo wao wa sita wa Europa League hatua ya Makundi dhidi ya wenyeji wao Zorya Luhansk katika uwanja wa Avanhard wenye uwezo wa kuchukua mashabiki zaidi ya 22000.
Man United ambao msimu huu hawana mwenendo mzuri katika mechi zao za msimu huu, wamefanikiwa kupata ushindi wa tatu katika michuano hiyo kwa kuifunga Zorya goli 2-0, ushindi huo unakuja wakiwa na kumbukumbu ya kushinda 4-0 katika mchezo wao wa Europa uliyopita dhidi ya Feyenoord.
Ushindi wa Man United ulianza kupatikana dakika ya 48 kupitia kwa Henrikh Mkhitaryan aliyepachika goli la kwanza na dakika ya 88 msweden Zlatan Ibrahimovic akapachika goli la pili, matokeo hayo yanawafanya Man United kumaliza nafasi ya pili katika msimamo wa Kundi A na kufanikiwa kutinga hatua inayofuata.
https://youtu.be/j3YKV4ryaLo
ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0