Leo December 21 2016 moja kati ya habari za michezo za kimataifa ambazo zimeagonga headlines ni kuhusiana na habari zilizoripotiwa na The Guardian kuwa wamiliki wa Man United ambao ni familia ya Glazer wanampango wa kumuongezea mkataba mpya Jose Mourinho.
Sky Sport wamefanya mahojiano maalum na Jose Mourinho na kumuuliza maswali mawili, moja ni kuhusu kuongezewa mkataba na uwezekano wa yeye kwenda China kufundisha soka, ikumbukwe kuwa Jose Mourinho alijiunga na Man United July 2016 kuchukua nafasi ya Louis van Gaal.
“Bado sijaambiwa kuhusiana na taarifa hizo na sitarajii kuona wakifanya hivyo sasa hivi, kwa sababu tayari walishanipa mkataba wa miaka 3 na wamekuwa wakinisapoti na kunifanya nijisikie kuwa sitakaa miaka mitatu pekee United kuwa nitaendelea kuwepo, kiukweli wakinipa mkataba sitafikiria mara mbili nitasaini”
“China ni sehemu ambayo inaweza kumvutia kila mmoja lakini napenda kufundisha soka la kiwango cha juu, bado nina umri mdogo nina miaka 53 bado nina miaka mingi ya kufundisha soka sifikiri kwenda China nahitaji kufundisha soka sehemu sahihi na kushinda mataji naimani nipo mahala sahihi”
https://youtu.be/chKJCIYJMkA
ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3