Ni siku 118 zimepita toka waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo Nape Moses Nnauye kutangaza kuufungia uwanja wa Taifa Dar es Salaam kutumiwa na timu za Simba na Yanga kutokana na uharibifu uliojitokeza wakati wa game yao, leo ametangaza maamuzi mapya.
Waziri Nape leo January 27 2017 kupitia wizara yake imetolewa taarifa za kuruhusu uwanja huo kuendelea kutumika kwa club zote ambapo baada ya kujiridhisha na ukarabati uliofanywa na club hizo za Simba na Yanga hivyo mechi ya Simba na Azam FC kesho itachezwa uwanja wa Taifa.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri waziri Nape alitangaza maamuzi ya kuufungia uwanja wa Taifa Jumapili ya October 2 2016 kutokana na uharibifu na uvunjifu wa viti uliofanywa na mashabiki wakati wa mechi hiyo ikiwa ni baada ya Amissi Tambwe kuifungia Yanga goli lililotajwa kuwa la utata.
ULIPITWA NA MAAMUZI YA WAZIRI NAPE KUHUSU YANGA NA SIMBA? TAZAMA HAPA