Kabla mwaka 2016 haujaisha na kuingia mwaka 2017 kuna mambo mengi ya kukumbuka katika soka kwa mwaka 2016, kama ni mfuatiliaji wa mchezo wa soka najua kuna habari nyingi sana ambazo zimepita na inawezekana zimeacha kumbukumbu katika kichwa chako, millardayo.com inakusogezea baadhi ya matukio 10 ya kukumbukwa kwa mwaka 2016.
1- November 29 2016 moja kati ya matukio ambayo hayatofutika katika soka ni ajali ya ndege iliyokuwa imebeba wachezaji wa timu ya Chapecoense ya Brazil waliyokuwa wanaelekea Colombia kucheza mchezo wa fainali ya kwanza ya Sudamericana, ajali hiyo iliua watu zaidi ya 70 kati ya 81 waliyokuwemo katika ndege hiyo.
2- Kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka Tanzania TFF April 3 kupitia kwa makamu mwenyekiti wake Jerome Msemwa walitangaza kufungia watu kujihusisha na soka maisha kutokana na tuhuma za upangaji wa matokeo zikihusisha michezo ya Kundi C iliyokuwa na timu za Geita Gold, Polisi Tabora na JKT Kanembwa.
3- January 8 2016 kwa mara ya kwanza katika historia ya soka Tanzania mtanzania Mbwana Samatta alifanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora Afrika 2015 kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani ya Afrika, Samatta alishinda tuzo hiyo akiwa anaichezea TP Mazembe.
4- January 24 2016 mtanzania Mbwana Samatta alisaini rasmi kuichezea timu ya KRC Genk ya Ligi Kuu ya Ubelgiji, timu ambayo imemfanya Samatta kuwa mtanzania wa kwanza kucheza hatua ya 32 ya michuano ya Europa League.
5- April 22 2016 mtanzania Farid Musa alipata nafasi ya kwenda Hispania kufanya majaribio katika timu ya Tenerife ya Ligi daraja la kwanza Hispania, Farid alifuzu lakini alilazimika kusubiri upatikanaji wa vibali hadi December 28 ndio akaondoka Tanzania.
6- Mwaka 2016 ni mwaka ambao timu ya taifa ya Ureno ikiongozwa na staa wao Cristiano Ronaldo ilitwaa taji la mataifa ya Ulaya kwa mara ya kwanza katika historia yao, hilo ndio taji lao kubwa la kwanza Ureno kuchukua.
7- Kama ni mtu wa michezo na unafuatilia Ligi Kuu England, basi najua huwezi kusahau tukio la timu ya Leicester City kutwaa taji la Ligi Kuu England msimu wa 2015/2016, Leicester hawakuwahi kufikiriwa kama wanaweza kutwaa Ubingwa na hususani msimu wa 2014/2015 walikuwa katika hatari ya kushuka daraja, Leicester hawakuwa wamewahi kutwaa Ubingwa wa EPL katika historia.
8- Mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal anayeichezea Shanghai Shenhua ya China Demba Ba huu ulikuwa ni mwaka mbaya katika soka baada ya kuvunjika mguu vibaya, kitendo ambacho wengi wamekuwa wakihisi kuwa anaweza akaachana na soka.
9- October 31 2016 taifa la Tanzania lilipokea taarifa mbaya kuhusu bondia Thomas Mashali ambaye alipoteza maisha kwa kuuwa na watu ambao inadaiwa kuwa walimuitia mwizi maeneo ya Kimara, Mashali alikuwa ni moja kati ya mabondia mahiri Tanzania.
10- Kwa mwaka 2016 huwezi kusahau kuhusiana na headlines za mabadiliko ya mifumo ya vilabu vya Simba na Yanga, kwa Simba bilionea wa 21 Afrika Mohammed Dewji aliomba kununua asilimia 51 ya hisa za Simba kwa bilioni 20 kama Simba watakubali kuingia katika mfumo wa hisa, huku Yanga mwenyekiti wao Yusuph Manji akiomba kuikodi timu hiyo.
ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3