Kuelekea game ya watani wa jadi itakayochezwa Jumamosi ya February 25 2017, mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga Salum Mkemi ameongea na vyombo vya habari na kuitambia Simba kuwa watawafunga na kuonesha mataji yao mbele ya waandishi wa habari.
“Siku ya tarehe 25/02/2017 katika uwanja wa mkuu wa Taifa tutataka kuiondoa Simba katika Premier League kwa sababu tutawafunga na hawatorudisha timu kipindi cha pili, tunajua mashabiki wao watavunja viti, kocha wao Omog anayetaka makombe haya tunamwambia makombe haya yamefika Yanga”
ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1