April 4 2017 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan aliwaalika nyumbani kwake timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys na kupata nao chakula cha jioni kabla ya vijana hao kuondoka Tanzania.
Mualiko wa Mama Samia Suluhu ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo waziri mwenye dhamana ya michezo Dr Harrison Mwakyembe aliyepewewa fursa pia kuongea na vijana wa Serengeti Boys na kumkaribisha Makamu wa Rais.
Kabla ya hapo waziri Mwakyembe alieleza pia kusikitishwa kwake na TRA kuinyang’anya Serengeti Boys basi muda mchache baada ya kutoka hotelini na kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwa makamu wa Rais walipokuwa wamepewa mualiko maalum.
ALL GOALS: Taifa Stars vs Botswana March 25 2017, Full Time 2-0