Baada ya usiku wa March 24 kuchezwa mchezo wa Jamhuri ya Ireland dhidi ya Wales na kumalizika kwa sare tasa ya 0-0, huku mchezo ukimalizika kwa masikitiko kutokana na staa wa Everton aliyekuwa anaichezea Ireland Seamus Coleman kuvunjika mguu kutokana na rafu aliyochezewa na Neil Taylor.
Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA leo March 27 2017 limetangaza mambo mawili ikiwemo kumpa adhabu Neil Taylor lakini pia kuamua kumlipa mshahara Seamus Coleman kwa muda wote atakaokuwa nje ya uwanja wa akiuguza mguu wake.
Taylor baada ya mechi alipokea sifa za kipekee baada ya kuamua kufanya kitu kisichokuwa cha kawaida kwa kuamua kwenda katika vyumba vya kubadilishia nguo vya Ireland na kuwaomba msamaha wachezaji wote kwa kosa lililotokea, Coleman baada ya kufanyiwa upasuaji atakuwa nje ya uwanja kwa miezi sita na atakuwa akilipwa mshahara wake ule ule wa pound 50,000 kwa wiki.
Video ya tukio la Neil Taylor kumvunja mguu Coleman
https://youtu.be/jluTfi1tlpM
ALL GOALS: Taifa Stars vs Botswana March 25 2017, Full Time 2-0