Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kwa shirikisho la soka Tanzania TFF na kutomtangaza refa wa game ya Simba vs Yanga inayotarajiwa kuchezwa kesho February 25 2017 uwanja wa Taifa Dar es Salaam, leo TFF wameamua kumtangaza refa Methew Akrama kutoka Mwanza ndio atachezesha game hiyo.
Kupitia kwa afisa habari wa TFF Alfred Lucas amewatangaza refa na wasaidizi wake katika game hiyo, baada ya hapo AyoTV ilitaka kufahamu kwa nini wamechukua muda mrefu kumtangaza refa wa game hiyo tofauti na miaka ya nyuma?
“Mchezo ni kesho na utachezeshwa na Methew Akrama, sababu kubwa ya kuchelewa kumtangaza muamuzi wa game hiyo ni kumuandaa kisaikolojia ukimtangaza mapema timu za Simba na Yanga zina uzito wa aina yake mchezo wake ni mgumu lengo lilikuwa ni kumuandaa kisaikolojia”
FULL HD: All goals N’gaya vs Yanga February 12 2017, Full Time 1-5