Moja kati ya stori ambazo zimevutia watu wengi ni hii ya staa wa Bongofleva Dully Sykes kuweka wazi kuwa Baraka Da Prince aliwahi kumpigia simu Dully na kuomba ampe jina la kisanii, ndio Dully Sykes alipoamua kumpa jina la Prince, hiyo ni kutoka katika instagram account ya Dully.
“Kuna siku ila mwaka sikumbuki nilipata simu kutoka kwa kijana aliyejitambulisha kwa jina la BARAKA akanisalimia na kunambia anahitaji nimpatie jina ili alitumie kwenye sanaa….nikamuuliza anaishi wapi?…akanambia anaishi MWANZA”
“nikamwambia nitampatia jina moja kati ya majina yangu…..ndipo nikampatia “PRINCE nikamwambia ajiite ….BARAKA DA PRINCE na kweli….nashukuru mungu yamekuwa na amekuwa mmoja kati ya wasanii wanaonipenda na kuniheshimu…. @barakahtheprince_ nakupenda sana mdogo wangu”
AyoTV imempata Baraka Da Prince katika exclusive interview na kumuomba aelezee kuhusiana na ishu hiyo ilikuwaje hadi kumpigia simu Dully “Ni zamani sasa sijui Dully hata kakumbukaje hiyo stori, miaka mingi sana hata wimbo mmoja redio nilikuwa nasikia tu Dully Sykes anaweza kukuchagulia jina likakuwa”
FULL VIDEO:Show ya Alikiba na Dimpoz Las Vegas Marekani March 3 2017