Mfanyabiashara na Mbunge wa Geita vijijini Joseph Musukuma ametolea ufafanuzi kuhusu kuandika neno ‘vyeti feki’ katika moja kati ya mabasi yake yanayofanya safari zake kanda ya ziwa, millardayo.com imemtafuta Musukuma azungumzie ishu hiyo.
Musukuma ambaye ni mbunge mwenye elimu ya darasa la saba ni nini kimemfanya aandike maneno hayo ‘vyeti feki’ hususani katika kipindi hiki ambacho kumekuwa na tuhuma za baadhi ya watu kuhusishwa kutumia vyeti feki.
“Nina mabasi 11 katika idadi hiyo ya basi 10 zote zina picha ya Magufuli na Musukuma, sasa hiyo mpya iliyotoka imeandikwa tutamkumbuka Jakaya halafu ikawekwa vyeti feki chini ikaandikwa Bombardier wala sikuwa na maana yoyote “
“Wale waliyopiga hiyo picha kwa chini ilikuwa bado inaandikwa Bombardier kwa chini kwa hiyo ni maneno tu, tunayo picha ya Magufuli imeandikwa hatujaribiwi, tunayo picha ya Magufuli imeandikwa tuwalinde wamachinga, tunayo picha imeandikwa tuliwapa uhuru hamkuutumia sasa waliyochukua hiyo wangechukua na zile 10 sisi hatukuwa na maana yoyote mbaya”
VIDEO: Maamuzi ya JPM baada ya kufanya ziara ya kushitukiza bandari DSM