Leo December 11, 2018 Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa amewaomba Wafanyabiashara Wilayani humo kuchangia fedha kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuwezesha Wanafunzi 5984 ambao wamefaulu kuingia kidato cha kwanza Januari 2019.
DC Kisa ameyasema hayo wakati alipokutana na wadau wa elimu katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Korogwe hii leo.
Korogwe kuna uhaba wa vyumba 150 ambavyo ujenzi wake utagharimu zaidi ya Milioni 700 na kama vyumba hivyo havitapatikana idadi kubwa ya watoto watabaki nyumbani na kushindwa kuhudhulia masomo yao ya Sekondari.
CHIPUKIZI AZUNGUMZIA MASTAA WALIVYOMBANIA KOLABO KISA PESA