Kamati ya kudumu ya Bunge ya katiba na sheria imemshauri msajili wa vyama vya siasa nchini kuvifutia usajili vyama vyote vinavyokiuka sheria na kanuni za uendeshaji wa vyama vya siasa. Ushauri huo umetolewa Bungeni leo na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mohamed Mchengerwa.
Mchengerwa amesema …>>>”Kamati inashauri na kusisitiza kwamba ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ihakikishe kunakuwepo na usimamizi wa karibu wa kufuatilia na kuchunguza mienendo inayoharibu sifa na vigezo vya vyama vya siasa nchini na kwamba msajili asisite kukifutia usajili chama chochote cha siasa kitakachokiuka kanuni na taratibu za vyama vya siasa nchini”
Serikali imetaja mkakati mpya wa kupambana na dawa za kulevya