Mwanzoni mwa mwaka 2016 Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali, Msichana Initiative linalotetea haki za wasichana kupata elimu, Rebeca Gyumi alifungua shauri mahakamani kupinga kifungu cha 13 na 17 cha sheria ya ndoa kinachoruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 14 kwa kibali cha mahakama, na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi.
Maamuzi ya mahakama ni kwamba serikali kupitia kwa Mwanasheria Mkuu kujipanga ili kuvirekebisha vipengele tata ndani ya mwaka mmoja. Baada ya maamuzi hayo ya mahakama kuu Serikali ya Tanzania imewasilisha ombi la kukata rufaa uamuzi huo. Kwenye interview hii na Ayo TV, Rebeca Gyumi ameeleza kushtushwa na taarifa za serikali kukata rufaa…….
>>>’Tumeshangazwa sana kwa sababu tunafikiri kimsingi wakati tulikuwa tumeshapiga hatua moja mbele, rufaa hii inaturudisha hatua mbili nyuma na kutuachia maswali mengi sana kwamba serikali ina nia gani kwa watoto wa kike na watoto kwa ujumla hapa Tanzania‘
ULIKOSA HII YA REBECA GYUMI ALIVYOSHINDA KESI YA KUPINGA UMRI MDOGO WA NDOA KUOLEWA TANZANIA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI