Zikiwa zimepita dakika chache tangu kocha Rafa Benitez alipothibitishwa kuwa kocha mpya wa Real Madrid , taarifa mpya juu ya wachezaji watakaosajiliwa chini yake imeibuka .
Kocha huyo mpya alikutana na Rais wa Real Madrid Florentino Perez hapo jana usiku wakati wa chakula usiku na agenda kuu ya mkutano wao ilikuwa usajili wa wachezaji akiwemo kipa wa Manchester United David De Gea.
Kwa mujibu wa habari za ndani , Benitez ameidhinisha usajili wa De Gea na kinachosubiriwa ni mazungumzo rasmi baina ya Real pamoja na Manchester United ili kukamilisha usajili wa kipa huyo .
Real Madrid wamekuwa wakimfuatilia David De Gea kwa muda mrefu na inaonekana kuwa ni kiasi cha muda tu kabla ya usajili wa mchezaji huyo kukamilika japo Manchester United kwa upande mwingine wamekuwa wakihaha kumsainisha mkataba mpya .
Hivi karibuni United imeweka ofay a mshahara wa paundi 200,000 kwa kipa huyo oa ambayo hata hivyo bado hajaikubali na inaaminika kuwa moyo wake umeamua kuwa atajiunga na Real .
Kwa upande mwingine wachezaji wengi ndani ya Old Trafford wanaamini kuwa kipa huyo hatarejea klabuni hapo kwa msimu ujao na viongozi wa United akiwemo kocha Louis Van Gaal wameanza kufanya mipango ya kusajili kipa mwingine .