Aliyekuwa mgeni wa muda wa staa Justin Beiber, Lil Za, amehukumiwa miyaka mitatu ya kufanya shughuli za kijamii ikiwemo kufanya usafi, pamoja na faini ya dolla 1,600 kwa fujo alizozifanya akiwa nyumbani kwa staa huyo.
Lil Za, ambaye jina lake kamili ni Xavier Smith, ni msanii wa Hip Hop na alikamatwa mapema mwaka huu kwa kosa la kurushia mayai viza nyumba ya jirani wake Beiber na kusababisha uharibifu wa dolla 20,000 pamoja na kuchafua mazingira.
Aliposechiwa, Lil Za alikutwa na madawa ya kulevya aina ya Molly au kwa jina lingine, Ecstasy. Polisi wa Los Angeles huko nchini Marekani bado wanafanya uchunguzi kujua kama Justin Beiber pia alihusika na kama akipatikana na hatia basi, wameahidi kumchukulia hatua kali za kisheria.
Justin Beiber amezidi kujikuta kwenye wakati mgumu siku za karibuni baada ya kuhusishwa na matumizi ya madawa ya kulevya pamoja na utovu wa nidhamu uliokithiri. Wakili wa staa huyo, Shawn Holley amesikika akimtetea Beiber mara nyingi akisema, utoto unamsumbua lakini anajifunza kutoka kwa makosa yake na atabadilika.