November 8 2016 kampuni hodhi ya rasilimali za Reli ‘RAHCO’ ilitangaza zabuni kwenye mradi wa ujenzi wa reli ya umeme kiwango cha ‘Standard Gauge’ kipande cha Morogoro-Makutopora. Kampuni ya Yapi Merkezi Insaat ve Sanayi A.S ya Uturuki ilionekana kukidhi vigezovya kiufundi na kifedha.
Leo September 28 2017 Serikali ya Tanzania imetia saini mkataba wa pili wa kujenga reli mpya ya Standard Gauge yenye uwezo wa kusafirisha mizigo ya tani MILIONI 17 kwa mwaka. Reli itakuwa inapitisha treni za umeme zenye mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Prof. Makame Mbarawa amezungumza wakati wa utiaji saini wa mkataba huo na kusema ……>>>”watu wengi ukizungumza ujenzi wa reli wanafikiria reli inajengwa siku moja, ujenzi wa reli unachukua muda mrefu na unachukua hatua tano”
Unaweza kuitazama video hii hapa chini
Sababu za gharama ujenzi reli ya kisasa awamu ya pili kuwa juu tofauti na ya kwanza, Bonyeza play kutazama
Ulikosa hii? BENKI KUU: kuhusu hali ya huduma za kifedha Tanzania, bonyeza play hapa chini kuitazama