Rais anayemaliza muda wake Abdelmadjid Tebboune almechaguliwa tena kuwa rais mnamo Septemba 8 kwa 94.65% ya kura. Kati ya jumla ya kura milioni 5.6 “zilizorekodiwa, milioni 5.320 walimpigia kura mgombea binafsi” Tebboune, “yaani 94.65% ya kura,” ametangaza Mohamed Charfi, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi.
Uchaguzi huu ulikuwa na ushiriki mdogo. Siku ya Jumamosi mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi alitangaza “kiwango cha wastani cha ushiriki cha 48.03% saa 2:00 usiku, kulingana na takwimu ya awali”, ikilinganishwa na mwaka 2019 (39.83%). Mwaka huo, rais wa Algeria alishinda uchaguzi wake wa kwanza wa urais kwa 58% ya kura.