Viongozi wa Afrika hivi leo wamewasili nchini Ukraine kabla ya hapo kesho kuelekea Urusi, katika ziara inayolenga kujaribu kuwashawishi viongozi wa nchi hizo mbili kukubaliana kumaliza vita inayoendelea.
Ujumbe huo wa viongozi wa Afrika, unaongozwa na rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, utakuwa na mazungumzo na rais Volodymry Zelenky na Vladimir Putin kwa nyakati tofauti.
Wajumbe hao kutoka Afrika Kusini, Misri, Senegal, Kongo-Brazzaville, Comoro, Zambia na Uganda wanatarajiwa kuzuru nchini Ukraine na Russia kuanzia mwishoni mwa wiki hii katika harakati za kujaribu kumaliza vita vya muda mrefu vya miezi 16 vya Russia nchini Ukraine, na Putin amesema anapanga kutumia fursa hiyo kuzungumzia suala hilo.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anaamini kuwa Putin na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy wanakubaliana naye kuhusu “umuhimu wa kusafirisha nafaka barani Afrika kwa ajili ya kupunguza uhaba wa chakula,” msemaji wa Ramaphosa Vincent Magwenya alisema.
Bw Ramaphosa amekuwa msukumo katika kufanikisha safari hiyo, akipiga simu kwa Bw Putin na Bw Zelensky, na kumjulisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hatua alizopiga.
Ingawa sio Urusi na Ukraine ambazo zimeonyesha nia yoyote katika mazungumzo ya amani, wote wana nia ya ziara hii.
Wachambuzi wanaona mkutano huo kuwa kiashiria muhimu cha uhusiano wa Afrika na Urusi, lakini sio wa kiitikadi.
“Waafrika wanafanya biashara katika hili,” anasema Dk Vines, akibainisha kuwa wasiwasi mkubwa wa wapiganaji wa zamani wa msituni nchini Msumbiji ambao alikuwa amezungumza nao hivi karibuni ni gharama ya maisha kwa sababu ya “vita hivi vya mbali vya Ulaya”.