Vyombo vya habari nchini Iran vimetangaza kifo cha Rais Raisi katika ajali ya helikopta, licha ya tangazo hilo, mamlaka haijazungumzia ripoti hii hadi tukichapisha taarifa hii.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Mehr, rais wa Jamhuri ya Iran, Ayatollah Ebrahim Raisi, alipata ajali wakati akiwa katika majukumu yake ya kitaifa na kwa ajili ya watu wa Iran, taarifa hii pia imeripotiwa na vyombo vingine vya habari vya ndani ya nchi.
Juampili ya wiki iliopita, shirika la habari la serikali lilikuwa limeripoti kwamba helikopta iliokuwa imembeba Raisi ilikuwa imepata ajali katika eneo la Jolfa, Mashariki mwa jimbo la Azerbaijan, ajali ambayo ilisababishwa na hali mbaya ya hewa.
Shirika la habari la serikali IRNA katika taarifa yake lilieleza kuwa ajali hiyo ilitokea katika msitu Dizmar karibu na mji wa Varzaghan.