Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan amesema kuwa Israel itakabiliwa na “madhara makubwa sana” ikiwa itawapiga marufuku Waislamu wa Palestina kuingia katika maeneo matakatifu wakati wa mwezi ujao wa Ramadhani.
“Tunafikisha jumbe zetu kwa mamlaka husika kuhusu haja ya kuzuia uchochezi kabla ya mwezi ujao wa Ramadhani,” Erdogan aliuambia mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas mjini Ankara.
“Madai ya wanasiasa wenye itikadi kali wa Israel kuwawekea vikwazo Waislamu katika Haram Al Sharif ni upuuzi mtupu. Matokeo ya kuchukua hatua hiyo bila shaka yatakuwa mabaya sana.”
tzazama pia…