Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev amekubali kujiuzulu kwa Baraza la Mawaziri nchini humo siku ya Jumatano baada ya ongezeko la bei ya mafuta nchini humo kusababisha maandamano ya raia ambapo karibu Polisi 100 wamejeruhiwa.
Polisi walifanikiwa kuwatawanya waandamanaji siku ya Jumanne lakini yameendelea tena leo huku maelfu ya waandamanaji wakisonga kuelekea katikati ya mji wa Almaty.
Juhudi za vikosi vya usalama zilishindwa kuwatawanya waandamanaji kwa mabomu ya machozi na mabomu ya kutupa.
Maandamano yalianza baada ya Serikali kupandisha bei ya nishati ya mafuta ya petroli kuanzia mwanzo wa mwaka.