Korea Kusini imesema itaendelea na juhudi za kuimarisha mahusiano na Korea Kaskazini licha ya onyo kutoka Korea Kaskazini kwamba Uadui utaongezeka iwapo yatafanyika mazoezi ya pamoja ya Kijeshi kati ya Korea Kusini na Marekani.
Jana Jumapili Dada wa Kiongozi wa Korea Kusini Kim Jong Un alionya kuwa mazoezi hayo yaliyoandaliwa baadaye Mwezi juu yatavuruga kwa sehemu kubwa juhudi za kurejesha imani baina ya Korea hizo mbili na kuutia doa Uhusiano unaojaribu kuota mizizi.Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini imesema itashirikiana na Marekani kupanga namna mazoezi hayo ya kijeshi yatakavyofanyika huku ikizingatia kutoharibu juhudi za Kidplomasia za kudhibiti mradi wa Nyuklia wa Korea Kaskazini.
Korea Kaskazini inayatafsiri mazoezi hayo ya Kijeshi ya kila mwaka kuwa ni uchokozi na mara kadhaa imejibu kwa kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu na silaha za nyuklia.
AGIZO LA RC DSM ASEMA “MWANANCHI AKIKATAA KUVAA BARAKOA ASIPAANDE GARI/NI AMRI”