Rais Dkt. John Magufuli ameguswa na kifo cha aliyekuwa miongoni mwa Mawaziri 11 wa kwanza wa Tanganyika, Balozi Job Lusinde, aliyefariki dunia Alfajiri ya Julai 7 na kuwapa pole wanafamilia wote, huku akieleza ni kwa namna gani ataukumbuka mchango wake mkubwa kwa Taifa letu.
“Nimesikitishwa na kifo cha Mzee wetu Balozi (Mst) Job Lusinde, nawapa pole Familia, wana Dodoma na Watanzania, nitaukumbuka mchango wake mkubwa kwa Taifa akiwa Waziri, Balozi, Mdhamini wa CCM na Kiongozi wa Wazee Dodoma, pumzika salama Mtani wangu, kazi kubwa umeifanya vizuri”-JPM