Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amevikemea Virusi vya Corona huku akivitaja kuwa ni moja ya sababu ya kuchelewesha utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta baina ya Tanzania na Uganda
Magufuli amekemea virusi hivyo leo wakati wa uwekaji wa saini wa mkataba wa utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta, mbele ya Rais Museveni uliofanyika mkoani Geita, ambapo pia ametumia nafasi hiyo kumshukuru Museveni kwa uvumbuzi wa mafuta hayo.
“Mradi huu umechelewa na bahati mbaya wakati wanaendelea kujadili pakatokea Corona na ishindwe na ikalegee huko, ikawa inachelewesha, nani anapenda kufa kwahiyo hili licorona likaanza kukoromela huu mradi wetu wa mafuta” Rais Magufuli.
“Jana Mzee Museveni akanipigia simu ananiambia, pamoja na Corona ninaomba tumalizie huu mradi uanze, Corona isiwe sababu ya kuchelewesha maendeleo ya Watanzania na Waganda, akasema mimi nitakuja na barakoa nikamwambia njoo mradi haulali” Rais Magufuli