Aliyekuwa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mhe. Harold Nsekela ameagwa rasmi jijini Dodoma huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiongoza zoezi hilo
Mwili wa marehemu Jaji Harold Nsekela umeagwa katika viwanja vya Chinangali leo huku viongozi wa juu wa serikali ,wafanyakazi wenzake, wabunge, mawaziri sambamba na mawaziri wateule wakiudhuria zoezi hilo.
Marehemu Jaji Mhe. Harold Nsekela alifariki Dunia tarehe 06/12/2020 asubuhi, mjini Dodoma baada ya kuugua kwa muda Mfupi na mwili wake unatarajia kuwasili mkoani Mbeya katika viwanja vya Songwe majira saa nane mchana kwa ajili ya mazishi yatakaofanyika siku ya Alhamisi 10/12/2020.
Marehemu Jaji Harold Nsekela aliteuliwa kuwa Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma mwezi Desemba, 2016, wadhifa aliokuwa nao mpaka alipofariki