Rais Magufuli, ameagiza kuwa mtu yeyote atakayepokea vifaa vya kupambana na Virusi vya Corona, vikishapimwa na Maabara Kuu ya Tanzania na kukutwa vina Virusi vya hivyo, basi ashtakiwe na apewe kesi ya jinai.
JPM “Kwa mtu yeyote atakayepewa vifaa vya kuzuia Corona, halafu mkavipima mkakuta vina Corona, huyo mtu apelekwe kwenye kesi ya jinai, hata mauaji, Watendaji wajiepushe kupokea pokea, tutatengeneza Barakoa zetu na tutatumia vifaa ambavyo vitakuwa tested na Maabara zetu, Corona inaisha lakini tusije tukapandikiziwa”.
LIVE: RAIS MAGUFULI IKULU, “PIGA NYUNGU, MA-RC WANAJIFUKIZA NA PENSI”, SEASON 2 INAANZA JTATU