Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amewatunuku Digrii za Awali, Stashahada na Ashtahada kwa wahitimu 2796 katika Mahafali ya 53 ya duru la pili la chuo hicho yaliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akijiandaa kuwapatia vyeti Elizabeth B. Kway na Placidi Leonardi Lala, wahitimu wa shahada ya awali ambao wamefaulu daraja la kwanza kwa wakia (GPA) ya 4.8 ambao ni ufaulu wa juu kupita wahitimu wote 2796.
katika Mahafali ya 53 ya duru la pili la chuo hicho yaliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam . Bi. Kway amefuzu Digrii ya Awali ya Sayansi katika Sayansi za Takwimu Bima (Bachelor of Science in Acturial Sciences) wakati Bw. Lala amefuzu Digrii ya Awali ya Elimu Jamii katika Muziki (Bachelor of Arts in Music).
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na meza kuu wakiwa wamesimama wakati wa Wimbo wa Taifa katika Mahafali ya 53 ya duru la pili la chuo hicho katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Balozi Nicholaus Luhanga aliyepata kuwa Makamu Mkuu wa Chuo hicho (1980-1988) walipokuwa katika Mahafali ya 53 ya duru la pili la chuo hicho katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.