Rais Yoweri Museveni wa Uganda amezinduwa tiba ya majaribio ya kutibu Corona Virus kwa kutumia dawa asilia kutoka nchini humo.
Majaribio yalitakiwa kuzinduliwa mwaka jana lakini yalicheleweshwa na zoezi la upatkanaji wa kibali kutoka Baraza la Taifa la Sayansi na Teknlojia (UNST).
Inaelezwa kuwa, Wanasanayansi wa Uganda wametumia miti kutengeneza dawa hiyo na majaribio ya dawa hiyo yatafuata Muongozo wa Shirika la Afya Duniani (WHO).
Rais Museveni amelaumu Mataifa ya Afrika kutegemea Mataifa ya Ughaibuni kupata tiba na chanjo ya Corona badala ya kufanya utafiti kwa kutumia Wanasayansi wa mataifa yao wenyewe.