Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema ndani ya jamii zetu yapo makundi maalumu yenye mahitaji yanapaswa kuhurumiwa zaidi ikiwemo watoto hususani yatima kuwalea vema na kuwasaidia, wanawake hususani wajane kuna wajibu wa kuwasaidia, wazee hususani wazazi katika kuwahurumia pia na walemavu kuhakikisha kutafuta njia za kuwasaidia.
Rais Alhajj Dk.Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 08 Septemba 2023 baada ya kujumuika na waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika Msikiti wa Salum Mmaka Mti Ulaya, Mkoa wa Mjini Magharibi.