Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mhe.Dk .Hussein Ali Mwinyi anataraji kuwa mgeni rasmi wa tamasha la Vumba linalotaraji kufanyika Disemba 31 visiwani Zanzibar
Tamasha hilo linataraji kufanyika katika viwanja vya Kizingo ambapo kutakuwa na michezo mbalimbali ikiwemo kula samaki aina ya Jodari mwenye kilo 10 kwa viongozi mbalimbali wa serikali Zanzibar
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Shaaban Ally Othuman amesema kuwa mbali na matukio hayo ya kimichezo tamasha hilo limelenga kurejesha kwajamii hususani kwa watu wenye mahitaji maalumu visiwani Zanzibar