Rais wa Urusi, Vladimir Putin ametoa pendekezo la kuanzishwa kwa Shule za kufundisha lugha za Kirusi katika Nchi za Afrika kama njia mojawapo ya kudumisha ushirikiano kati ya Urusi na Afrika.
Putin amesema hayo wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Kimataifa la Uchumi na kibinadamu uliofanywa na Rais Putin kwenye Kituo cha mikutano na maonesho St. Petersburg nchini Urusi.
“Tunapendekeza tuanzishe Shule zitakazofundisha Kirusi katika Nchi za Afrika itasaidia sana na utakuwa msingi imara wa ushirikiano utakaonufaisha Watu wa Urusi na Afrika kwa pamoja kupitia fursa mbalimbali”