Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza Kijana aliyewaokoa Watu 24 kwenye ajali ya ndege Bukoba jana atafutiwe kazi kwenye Jeshi la Uokozi.
“Tukiwa hapa wakati RC anaongea na kutoa shukrani za pongezi, Rais ametupigia simu hapa na Rais ameagiza akabidhiwe kwa Waziri wa Mambo ya Ndani nae pia atafutiwe nafasi kwenye Jeshi la Uokozi ili Kijana huyu apate mafunzo zaidi wa ujasiri wake huo aingie kwenye Jeshi hilo ambalo linahitaji ujasiri aliouonesha” ——— amesema Waziri Mkuu Majaliwa