Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani Jijini Arusha leo June 25,2023 ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kwamba uchunguzi unaonesha ipo baadhi ya Mikoa ikiongozwa na Arusha ilipata umaarufu kwa kilimo haramu cha bangi.
“Arusha mmejisema wenyewe hapa Mkuu wa Mkoa kajisema mwenyewe na kwamba hili dude la arusha ni organic na ni kali mno lakini Mikoa mingine na naona Wakuu wa Mikoa wapo hapa Mara wamo kwenye hili , Manyara, Morogoro, Iringa , Ruvuma, Tanga na Kilimanjaro wote mmeathirika na balaa hili kwa kiasi kikubwa kwahiyo naomba wote mkaweke nguvu katika kuilinda Jamii na balaa hili”
“Nilikuwa nanong’ona na Waziri Mkuu wazo la kwamba zile fedha tulizositisha za 10% za Halmashauri kuzielekeza Halmashauri Vijana hawa (Waraibu waliokuwa wanatumia dawa za kulevya wakaacha) waunganishwe wakapate pesa wajue kile watakachoenda kukifanya, naomba Waziri Mkuu lisimamie hilo mkalipange vizuri”