Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo wakati akipokea Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) Ikulu Jijini Dar es salaam amehoji kuhusu mikopo chechefu na kusema kuna baadhi ya Maafisa wa Benki wanashirikiana na Wateja kupitisha mikopo kinyume na inavyotakiwa kisha.
“Kuhusu mikopo chechefu na yenyewe unajiuliza why mikopo chechefu?, hivi ingekuwa Benki zinazotoa mikopo ni Benki binafsi kwenye rekodi zao kungekuwa na mikopo chechefu?, kusingekuwa, wetu sisi wa Serikali wanashindwa nini mpaka kunakuwa na mikopo chechefu?, kuna ushirikiano baina ya Maafisa wa Benki na hao wanaoenda kukopa, andika nitakupitishia ukipata chako hiki changu hiki, hailipiki tunasema mikopo chechefu”
“Kuna Mtu Mfanyabiashara kakopa Benki zetu sita sijui tano Mabilioni kila Benki, kachukua fedha yetu kaitoa nje na yeye kaondoka, leo tunasema mikopo chechefu mlipompa huyu!, dhamana zote alizoweka ni feki, zote feki, kama sio ushirikiano kitu gani? lakini Watu wanazunguka tunawatazama, wapo na wanajua walichokifanya, hii mikopo chechefu itachechemea mpaka tujirekebishe na inapochechemea na Nchi inachechemea” ——— Rais Samia.