Rais Samia Suluhu Hassan amepongeza jitihada za Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) katika kuendeleza sekta ya afya hapa nchini kupitia huduma za kibenki pamoja program zake mbalimbali zinazolenga kuboresha sekta hiyo muhimu.
Pia ameiomba benki hiyo kuangalia namna itakavyoweza kusaidia ufadhili wa masomo ya wataalamu wa afya kwa watoto wenye hali usonji nchini.
Rais Samia ametoa pongezi hizo leo Jumatano wakati akihitimisha Kongamano la Rasilimali Watu wa Sekta ya Afya lililoandaliwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Kongamano hilo limehudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya afya pamoja na viongozi waandamizi wa kitaifa akiwemo Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Hussein Ally Mwinyi, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na viongozi wengine wa serikali wakiwemo wastaafu.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Rais Samia alionyesha kuridhishwa zaidi na jitihada za benki za benki ya NBC katika kuhudumia kuhudumia wadau mbalimbali wa sekta ya afya kupitia mikopo isiyo na riba sambamba na kufadhili programu mbalimbali kwenye sekta hiyo ikiwemo ile ya ufadhili wa masomo kwa wakunga 100 inayotekelezwa na benki hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Benjamin Mkapa.
“Nimefurahishwa na jitihada za NBC ambao wametoa katika hisani yao kurudhisha kwa wananchi na ndio waliosomesha wale wakunga 100 kwa kushirikiana na taasisi ya Benjamin Mkapa…sasa niwaombe jitihada hizi ziendelee zisiwe za mwaka mmoja. Niombe jitihada hizo ziendelee kusomesha wataalamu kwenye fani ambazo taasisi na Wizara wataona zinastahili zaidi. Tumeskia Waziri wa Afya amesema kuna uhaba wa wataalamu kwenye eneo la Watoto wetu wenye hali ya usonji naomba sasa mjjielekeze kusomesha hao wawe wengi,’’ alisema Rais Samia.
Pongezi hizo za Rais Samia zimekuja siku moja baada ya pongezi kama hizo kutolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea banda la Maonyesho ya huduma za benki hiyo mahususi kwa wadau wa afya lililopo kwenye viunga vya mkutano huo.