Rais Samia Suluhu Hassan amesema hakuna aliye mkubwa zaidi ya sheria za chi, akiagiza kuchukuliwa hatua dhidi ya wote wanaodaiwa kutunishia misuli wakuu wa wilaya na mikoa kwa kuingiza mifugo kwenye ardhi oevu.
Akizungumza jana wakati wa hafla ya ufungaji lango litakaloruhusu maji kuanza kujaa kwenye Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme la Nyerere (JNHPP), Rais Samia alisema manufaa ya bwawa hilo yataonekana endapo vyanzo vinavyopeleka maji vitatunzwa.
Alisema Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango, alitoa maelekezo ya kuondolewa kwa mifugo yote kwenye Bonde la lhefu, huku akiwataka wakuu wa mikoa kusimamia kikamilifu a uwezo wa vijiji uangaliwe kabla ya kupeleka mifugo huku kukiwa na msisitizo wa kufuata sheria na kanuni ikiwamo kuzingatia haki za binadamu katika utekelezaji wake.
“Tuna uzoefu wa mapigano ya wakulima na wafugaji katika Wilaya ya Kilosa, Mkuu wa Wilaya alipoulizwa ‘kwanini kwako kuna wengi wanakufa kutokana na matukio haya?’ alisema ‘ng’ombe wengi wanaoingizwa ni wa wakubwa, nami siwezi kuwagusa’.