Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amechangia mjadala wa kupitisha azimio la serikali kuhusu mapendekezo ya kuridhia mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa Bandari Tanzania ambapo amesema manufaa ambayo yanatarajiwa kupatikana iwapo Bunge litaridhia azimio hilo ni pamoja na kuongezeka kwa Mapato ya Serikali.
“Kwenye kumbukumbu sidhani kumewahi kuwa na majadiliano ya mkataba yaliyohusisha watanzania wengi kama haya. Watanzania wengi wamejadili kwenye platform mbalimbali. Kwenye mitandao ya kijamii ndani na nje ya nchi yetu. Kwenye vyombo vya habari, barabarani na kwingine kote. Na hapa inathibitisha namna ambavyo Rais Samia Suluhu Hassan amejenga mazingira bora mazuri na salama ya Watanzania kutoa maoni yao bila woga wala hofu.”Mheshimiwa Nape Nnauye Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.