Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan amekabidhi vyakula pamoja na vitoweo kwa vituo 2 ikiwemo kinacholea watoto watokao katika mazingira hatarishi ikiwa ni katika kusherehekea sikukuu za krismasi na mwaka mpya huku akivitaka vituo hivyo kulea watoto hao katika maadili.
Hayo yamebainishwa na Msaidizi wa Rais katika masuala ya Siasa, Benedicta Kiyove katika moja ya kituo kilichopo Msimbazi Center jijini Dar es Salaam huku akisema vituo vilivyokabidhiwa vyakula na vitoweo hivyo ni kutoka Dar es Salaam pamoja na Dodoma huku akisisitiza kuwa ujumbe wa Rais Dkt Samia amesisitiza malezi bora yenye kuzingatia maadili kwa watoto.
Naye Mwakilishi wa Kituo cha Kulea Watoto waishio katila mazingira hatarishi katika eneo la msimbazi Sista Stella amemshukuru Rais Dkt Samia kwa msaada huo kwani utawafanya kusherehekea sikukuu za Noeli na Mwaka Mpya kwa amani na faraja kubwa ndani yao.