Rais Samia ametuma salamu za pole kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo kufuatia kifo cha Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Elias Kwandikwa kilichotokea August 02,2021 Jijini Dar es salaam.
Rais Samia amesema amepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Kwandikwa ambaye ni Mbunge wa Ushetu Mkoani Shinyanga kutokana na mchango wake mkubwa katika Utumishi wa Umma.
“Tumempoteza Mtu muhimu ambaye mchango wake katika utumishi wa Umma hautosahaulika , Kwandikwa alikuwa Kiongozi shupavu ambaye alikuwa akitekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria na taratibu”———Rais Samia
KIFO CHA WAZIRI WA ULINZI TANZANIA, RIDHIWAN KIKWETE ATOA NENO “PUMZIKA MWANAJESHI”