Rais Samia amempa Mariam Mwakabungu (25) shilingi milioni mbili kama shukrani na pongezi kwa kujitolea kuokoa maisha ya Watoto wachanga (Njiti) waliokimbiwa na Mama zao katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana kwa kuwakumbatia ili wapate joto na kuongeza uzito.
Mganga Mfawidhi wa Amana, Dkt. Bryson Kiwelu amesema hadi sasa Watu mbalimbali wameguswa na anachokifanya Mariam akiwemo Rais Samia na kuwataka wengine wajitokeze kufanya kazi hiyo.
Ripota wa Ayo TV, Bakari Chijumba ameongea na Mariam baada ya kupewa fedha hizo na kusema amejisikia furaha sana na kumshukuru Rais Samia “sikutegemea, nimeona kama ndoto sikujua litafikia huku”
Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundatin, Doris Molllel @dorismollel amempa pia pesa Mariam ambaye halipwi chochote na amekaa Hospitalini hapo kwa mwezi mmoja sasa akifanya huduma hiyo na kuomba Watanzania mbalimbali kumpongeza Mariam kwa kumtumia chochote kwenye 0782124700 (Alise Mwakabungu)