Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Injinia Deusdedit Kakoko kupisha uchunguzi .
Rais Samia amefanya maamuzi haya baada ya kupokea Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2019/2020 ambayo imeonesha ubadhirifu mkubwa Bandarini.
“Kuna ubadhirifu mkubwa Bandarini naomba TAKUKURU ikafanye kazi, nimeletewa ripoti ya ubadhirifu wa Bilioni 3.6 ” – Rais Samia.
“Imani yangu ni kwamba ndani ya Shirika la Bandari kuna ubadhirifu kama wa Tsh. Bilioni 3.6 lakini Waziri Mkuu amefanya ukaguzi na waliosimamishwa ni wa chini, nimeomba mara moja nitoe agizo la kumsimamisha Mkurugenzi Mkuu wa Bandari halafu uchunguzi uendelee” – Rais Samia Suluhu.
ULIPITWA? TAZAMA HAPA RAIS SAMIA SULUHU AKIPOKEA RIPOTI YA CAG NA KUZUNGUMZA.