Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameawapisha Viongozi wateule Ikulu jijini Dar es Es Salaam leo tarehe 14 Julai, 2023.
Miongoni aliyoyazungumza ni kuhusiana na yale yanayoendelea mitandaoni juu ya Uwekezaji wa Bandari.
‘Wakati sisi tunalumbana, bandari apewe nani, wenzetu kwa kuona malumbano yetu “wame-jump” wameenda kulekule, na lilelile jumba lililowekwa bendera ya Tanzania, limewekwa bendera ya jirani’- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
‘Sasa (kama) Tanzania tumeuza wale jirani wamekimbilia kule kufanya nini?, na siku ambayo Bunge letu limesema kwamba ni ruhusa bandari iendeshwe na Serikali na sekta binafsi, siku ya ya pili wenzetu wakasema ninyi moja, sisi zote zilizoko huku ziende sekta binafsi na wakakimbia kule kwenda kuwahi nafasi kama wale wanalumbana njooni huku.
Sasa muone jinsi fursa zinavyokuja na kukimbia haraka na jinsi wengine wanavyoweza kuzitumia harakaharaka.” -Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan