Rais Samia Suluhu Hassan ametoa msamaha kwa Wafungwa 5,704 katika kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru, akizungumza na Wandishi wa Habari Waziri wa Mambo ya Ndani ya Tanzania George Simbachawene amesema Rais Samia ametoa msamaha huo kwa masharti ikiwa ni pamoja na Wafungwa hao kutakiwa kuwa wametumikia robo ya adhabu zao gerezani na wawe wameingia kabla ya Oktoba 9, 2021.