Rais Samia Suluhu Hassan leo Ikulu Dar es salaam amesema anafurahishwa na juhudi zinazofanywa na Wizara ya Ardhi chini ya Waziri wake @JerrySilaa kupita kwa Wananchi kusikiliza kero zao na kuzitatua palepale bila kuzisubirisha.
“Migogoro ya ardhi imekuwa mingi sanasana Watu hawana raha kwa migogoro ya ardhi, nilikuwa nimesoma andiko moja Wiki iliyopita limeandika Nchi za Kiafrika ambazo Watu wake wana furaha Tanzania ya nne, nikasema mmmh ngoja nisome kilcholeta furaha ni nini!?, nikasoma huko ndani hawakendwa deep lakini wamesema tu Tanzania wa nne, sasa kama tupo wanne tupimwe zaidi basi twende juu, Watu hawana furaha, akilima hivyo, asipovuna hivyo, sijui akipata fedha yake hivyo, pesa ya Serikali inaingizwa akaondoshe shida yake haifiki” ——— Rais Samia.
“Ardhi zao zinanyang’anywa kuna Wababe wao wanajifanya ni Master ardhi wananyang’anya ardhi za Watu niwaombe sana simamieni, ardhi ndio msingi wa kila kitu, ardhi ndio utajiri wa Mtu, wale wanaokusanya tu ardhi za Watu jamani yana mwisho, nendeni kasimamieni kero za ardhi”
“Nafurahishwa na juhudi zinazochukuliwa sasa hivi na Wizara ya Ardhi kupita na kusikiliza kero na kuzitatua palepale lakini Wizara ya Ardhi ni moja Waziri ni mmoja na Timu yake ndio anaiburuza wanakwenda, jana nilikuwa nao nimewapa maneno yaoo nadhani mtawaona huko sasa wanachemka wanakuja angalau wameanza kuonesha lakini hawa hawawezi kufanya kazi kila mahali, Wakuu wa Mikoa wasaidieni angalau wakija wanakuta mmeshafanya wao wanatoa suluhisho” ——— Rais Samia. #MillardAyoUPDATES