Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutanoi Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa na Wadau wa Demokrasia katika ukumbi wa JNICC leo tarehe 11 Septemba, 2023 katika viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Tumeruhusu mikutano ya hadhara tukiwa na nia ya vyama vya siasa vizungumze, wananchi wasikie sera, mada na mipango yao ili vyama vikue na kurudisha wale waliowapoteza ili tukienda kwenye uchaguzi kila chama kimejijenga vya kutosha, hatukutoa fursa ile watu wavunje sheria, watu wakasimame kutukana, kukashfu, watu wakasimamme kuchambua dini za watu,”- Rais Samia Suluhu
“Lakini sishangai kwanini haya yanatokea, kwa sababu ya kuzungumzwa hakuna, tulianza ooh na Katiba, ikakatika katikati, ikaja bandari imeenda, sasa Katiba tena, niwaombe sana vyama vya siasa tumieni fursa kajijengeni kwa wananchi, ili wananchi warudi wawaunge mkono,
“Rais Samia mwingine kaumbwa hivyo roho yake basi tu, raha zake aone ugomvi mabishano hivyo, na huyo amua leo mwambie mimi nakupa serikali na wenzio hao, ataunda chama chengine awapinge wale wenzie aliokuwa nao, na ndiyo tunayoyaona huko kwao, ukiona hawapo hapa sio tu kwamba labda kuna kununa, huko kwao ndani hakukaliki ndani kuna moto,”- Rais Samia Suluhu Hassan
“Uhuru wa kutoa maoni una mipaka yake, kama ulizaliwa na Baba yako na Mama yako ukalelewa vyema, ukapitishwa kwenye mafunzo ya dini maneno mengine huwezi kuyasema, mengine tunayoyashuhudia kwenye mitandao aliyelelewa vizuri hawezi kuyasema, si wote tumepata bahati hiyo, wengine wamechipuka tu hivyo wameona dunia ndiyo hii hapa, wakawa kama kipofu kaona jogoo kila unachomuambia anaitikia kama jogoo, kumbe aliona jogoo macho yakafumba tena, anachokijua duniani ni jogoo tu,”– Rais Samia Suluhu Hassan