ais Samia leo wakati akipokea ripoti ya CAG Ikulu, Chamwino, Dodoma amesema Serikali za Mitaa bado kuna upotevu mkubwa wa mapato ambapo amemtaka Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa kuwa mkali na kutowahurumia wanaoiba fedha za Serikali.
“Waziri Bashungwa endelea kusimamia, ni kweli kuna waliofariki au ambao wamestaafu na wengine wamefukuzwa kazi lakini bado mishahara ipo, inaonesha bado wanalipwa mishahara”
“Inno (Waziri Bashungwa) usione shida kufukuza wale ambao una uhakika wameiba, msiwaonee huruma waende wakaonje maisha nje kuna Vijana wengi wanataka hizo nafasi, anayeharibu fedha za Serikali muweke pembeni akaonje maisha nje chukua mwingine aliye nje weka hapo ndani, tusileane, ukiwalea wanasema anayehofia Mtoto kulia analia yeye, sasa Inno ukiwaonea huruma utakuja kulia wewe and am serious on that”.