Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameungana na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema, kuweka mashada ya maua kwenye Mnara wa uhuru wa Zambia.
Rais Samia ameweka shada hilo ikiwa ni ishara ya kutoa heshima na kutambua walioongoza harakati za kuliltea uhuru Taifa hilo mwaka 1964.
Baada ya kuweka shada kwa mashujaa, Rais Samia pia ameweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa la Zambia, Dk. Kenneth Kaunda jijini Lusaka.
Leo Zambia inaadhimisha miaka 59 tangu ipate Uhuru kutoka kwa Waingereza mwaka 1964 na tukio la kuweka shada hufanywa kila mwaka wakati wa maadhimisho haya.
Rais Samia amealikwa kuwa mgeni rasmi kwenye tukio la maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru litakalofanyika baadaye leo kwenye Ikulu ya Zambia.