Rais wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza mkutano wa siku mbili wa Baraza la usalama la umoja wa Afrika huku kama nchi (Tanzania) ndio Mwenyekiti wa Baraza hilo kwa mwezi mmoja wote wa mei.
Akiongea na waandishi wa habari Waziri wa Mambo ya Nje January Makamba amesema kama nchi imepewa fursa ya kuandaa kumbukizi ya miaka 20 ya tangu baraza hilo lianzishwe mwaka 2004 na sherehe hizo zitafanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam
Aidha amesema viongozi mbalimbali wa nchi za afrika watahudhulia mkutano huo utakaoanza Mei 24 na 25 huku Rais wa Gambia,Msumbiji,Uganda na Marais wengine wastaafu wa Afrika wakiongozwa na Dr Jakaya Kikwete na Chisano wa msumbiji wakialikwa katika mkutano huo wa Baraza la Amani la Umoja wa Afrika.