Rais Cyril Ramaphosa amewasili Ukraine Ijumaa asubuhi kwa mujibu wa akaunti za mitandao ya kijamii za Ofisi ya Rais licha ya timu yake ya usalama kuzuiliwa nchini Poland.
Kulingana na Mkuu wa Huduma za Ulinzi wa Rais, Meja Jenerali Wally Rhood, maisha ya Ramaphosa siku ya Alhamisi “yalikuwa hatarini” baada ya washiriki waliofunzwa sana wa timu yake ya ulinzi waliokuwa na nia ya kutoa ulinzi mkali kwa rais mjini Kyiv, Ukraine, kukwama kwenye ndege nchini Poland. kutokana na kanuni za usafiri wa anga na urasimu.
Waandishi wa habari wa Afrika Kusini waliripoti kuwa Poland iliwanyima kuingia baadhi ya wanachama wa timu ya usalama ya Afrika Kusini walipowasili Warsaw.
Mkuu wa usalama wa Ramaphosa, Meja Jenerali Wally Rhoode, ilisema serikali ya Poland inahatarisha usalama wa rais kwa kutowaruhusu kuendeklea na safari.
“Wanatuchelewesha, wanaweka maisha ya rais wetu hatarini,” aliwaambia waandishi wa habari. “Kwa sababu tungelikuwa Kyiv kwa sasa lakini wameamua kutufanyia hivi. Nataka mujioneee jinsi walivyo wabaguzi wa rangi.”
Mamlaka ya Poland haijatoa maoni yoyote kuhusiana na sualahilo ambalo limegeuka kuwa mzozo wa kidiplomasia – ingawa haijamzuia Bw Ramaphosa mwenyewe kuelekea Kyiv, ambako aliwasili kwa treni Ijumaa asubuhi.
Alipokelewa katika mji mkuu wa Ukraine na balozi wa Afrika Kusini na mjumbe maalum wa Ukraine katika Mashariki ya Kati na Afrika, kulingana na urais wa Afrika Kusini na baadae atasafiri hadi Urusi katika azma ya Afrika ya kusuluhisha mzozo huo.
Ukraine imesema mara kwa mara haitoanzisha mazungumzo ya amani na Urusi hadi pale majeshi ya Urusi yatakapoondoka katika eneo lililokaliwa kwa mabavu, na majukumu ya Mkataba wa Roma wa Pretoria yametiliwa shaka huku kukiwa na wasiwasi kwamba Afrika Kusini haitamtia nguvuni rais huyo wa Urusi kwa waranti ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ikiwa atasafiri kwenda Afrika Kusini mwezi Agosti kwa ajili ya mkutano wa kilele wa BRICS mwaka huu.
Msemaji wa Ofisi ya Rais Vincent Magwenya alitoamaoni yake juu ya maoni ya afisa mkuu wa Rais Cyril Ramaphosa Jenerali Wally Rhoode kuhusu masuala ya usalama wakati wa ujumbe wa amani wa viongozi wa Afrika barani Ulaya.
“Ningependa kuwahakikishia Wa-Afrika Kusini wote kwamba hakujakuwa na maelewano yoyote kwa usalama wa rais kutokana na mzozo uliohusisha ukodishaji wa ndege na timu ya Huduma za Ulinzi wa Rais na vyombo vya habari,” Magwenya alisema Ijumaa.
Alitweet akisema Ramaphosa aliwasili salama mjini Kyiv, Ukraine, kwa treni pamoja na wakuu wengine wa nchi na serikali ambao ni sehemu ya ujumbe wa amani wa Afrika kwa Ukraine na Urusi.